Skip to Content

DCJ inataka kujenga jumuiya zilizo na nguvu katika NSW kwa kusaidia watu katika jamii yetu ambao wanahitaji msaada zaidi.

Tunafadhili mipango ya kusaidia watoto na familia, watu wenye ulemavu, na wazee.

Tunasaidia watoto walio na mazingira magumu, vijana na familia.

DCJ ina jukumu (la kisheria) la kulinda watoto na vijana katika NSW kutokana na hatari ya madhara makubwa. Ili kufikia hili, tunafanya kazi kwa karibu na idara nyingine za serikali za NSW, mashirika yasiyo ya serikali (NGOs) na jamii.

Tunatoa fedha kwa mashirika ambayo yanasaidia watoto na familia. Msaada huu unajumuisha mipango yenye:

  • kusaidia wazazi wapya wanao sumbuka na maisha
  • kufundisha malezi mazuri kuunda familia zenye nguvu
  • kusaidia wazazi wanaokabiliana na tatizo la pombe na matumizi mengine ya dawa za kulevya
  • kusaidia familia kusimamia masuala ya afya ya akili, ulemavu wa akili au matatizo ya kujifunza.

DCJ hutoa huduma kwa watoto na vijana ambao hawana usalama kuishi nyumbani. Hii inatiya ndani huduma ya kuwapa watoto watu wainje wakuwalea au watu walio na uhusiano wa kifamilia nao wakuwalea. Tunasaidia pia mtoto kupewa mzazi mupya kulingana na sheria, uangalizi na chaguzi za kudumu za malezi ili kuhakikisha watoto hupata mwanzo bora uwezekanao katika maisha.

Ikiwa una wasiwasi kwamba mtoto iko anaumizwa au hana usalama nyumbani, unaweza ita Child Protection Helpline  (Usalama wa Watoto) wakati wowote, mchana au usiku, siku 7 kwa wiki kwenye namba 13 21 11.

Tunasaidia watu wanaoathirika na unyanyasaji wa ndani na wa familia.

Ikiwa mwenzi wako, mume, baba au mtu mwingine nyumbani anakuhofisha na anakutukana au analeta vurugu kwako au kwa watoto wako, unaweza kuomba msaada. Namba ya Domestic Violence Line (Vurugu za Nyumbani) 1800 656 463 inafunguliwa masaa 24 kwa siku, siku 7 kwa wiki.

Pia tunatoa msaada kwa watu ambao wameponyoka unyanyasaji wa nyumbani na wa familia ikiwa ni pamoja na usaidizi unaoitwa Staying Home Leaving Violence (Kukaa Nyumbani Kuacha Vurugu) na pia Start Safely (Anza Kwa Usalama).

Ikiwa wewe ni mzee (kwa kawaida ukiwa na miaka zaidi ya 65) ambaye hunyanyaswa au unawasiwasi kuhusu mtu mwingine mkomavu ambaye anaweza kuwa ananyanyaswa, tafadhali pigia simu Elder Abuse Helpline (Huduma ya Usaidizi kwa Wazee Walionyanyaswa)  na Kituo cha Rasilimali kwenye namba 1800 628 221.

Ikiwa unahitaji mkalimani, kwanza piga simu 131 450, kisha uambie mtu wa mapokezi lugha yako na uombe ufikiaji wa Elder Abuse Helpline. Elder Abuse Helpline ni huduma pasipo malipo, ya siri ambayo hutoa ushauri na uhamisho wa kusaidia watu wakubwa wanao kabiliana na unyanyasaji.

Tunatoa msaada wa makao na msaada kwa watu wanaostahiki.

Tunatoa msaada na huduma kwa watu wanaohitaji msaada wa makao na wenye kufikia vigezo vya ustahiki. Huduma zetu ni pamoja na:

  • msaada wa kifedha kwa watu wanaohangaika na kulipa kodi au ambao wanataka kuanza kukodisha
  • kutoa maeneo ya kuishi ya gharama nafuu ya kuishi kwa watu wenye kipato cha chini hadi cha wastani ikiwa ni pamoja na makao ya umma, nyumba za jamii na nyumba za Waaboriginal. Aina hii ya msaada wa nyumba unaitwa "nyumba ya jamii"
  • mipango ya kuwasaidia watu wanaoishi katika nyumba za  jamii wanatekeleza mengi katika maisha.

Utahitaji kufikia vigezo vingine vya kustahiki ili ufikie huduma. Kwa habari zaidi, ita Housing Contact Centre (Kituo cha Usaidizi wa Nyumba)  kwenye  1800 422 322.

Ikiwa unahitaji mahali pa kukaa kwa muda mfupi kwa sababu huna makao au uko kwenye  hatari ya kukosa makao, piga simu kwenye Link2Home wakati wowote, mchana au usiku 1800 152 152.

Nambari za simu kwa usaidizi wa haraka

HaliWasilianaMda
Ikiwa huna nyumba au unahitaji mahali pa kukaa kwa muda mfupi Link2Home
1800 152 152
24/7
Vurugu za nyumbani na familia NSW Laini ya unyanyasaji wa ndani
1800 656 463
24/7
Ripoti unyanyasaji wa watoto au kutokujali watoto. Huduma ya Usaidizi wa Watoto
13 21 11
24/7
Mtu mzee ambaye yuko kwenye hatari Laini ya Msaada kwa Wazee wanao nyanyaswa
1800 628 221
Jumatatu hadi Ijumaa 8.30am - 5pm
Dharura NSW Polisi au Ambilansi
000
24/7

Huduma za utafsiri na ukalimani

Ikiwa unataka kutumia huduma za DCJ lakini huzungumzi Kiingereza au ukiwa na ugumu wa kuzungumza Kiingereza, tumia huduma za utafsiri na ukalimani bila malipo.

Kwa masuala ya makao:
Huduma ya All Graduates ya Utafsiri na Ukalimani: 1300 652 488
(All Graduates itawapigia watoa huduma wa nyumba na kukusaidiya na ukalimani bila malipo).
Ili kujifunza zaidi, tembelea tovuti ya All Garuates: http://www.allgraduates.com.au

Kwa mambo mengine:
Translating and Interpreting Service (TIS National)  (Huduma ya Utafsiri na Ukalimani (TIS Nationa): 131 450
(Huduma hiyi hufunika lugha zaidi ya 150. Hii ni huduma bila malipo).
Ili kujifunza zaidi, tembelea tovuti ya TIS: https://www.tisnational.gov.au

  • DCJ ina wajibu wa kutoa wakalimani walio hitimu wakati wa mahojiano na kuzungumza juu ya mambo magumu au masuala nyeti.
  • Katika hali nyingi, familia na marafiki hawawezi kutenda kama wakalimani lakini wanaweza kukaa wakati wa mahojiano au mkutano ili kutoa msaada.
  • Mwana memba wa familia au rafiki anaweza kufanya kazi  kama mkalimani ikiwa DCJ haiwezi kupata mkalimani aliye hitimu kwenye simu ao macho kwa macho.
Was this content useful?
Your rating will help us improve the website.
Last updated: 20 Mar 2023